Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kwanini shinikizo la juu la damu limekuwa likiwakumba watu wengi, maradhi haya zaidi yanatokana na mtindo wa maisha namna tunavyokula na jinsi tunavyokunywa. Hapa nitakupatia baadhi ya vyakula ambavyo utavitumia ambavyo ni rahisi kupatikana kwa wingi katika mazingira na masoko yetu
Je ni vya kula vipi utumie?
Ili moyo uwe imara unapaswa kula kwa wingi vyakula vyenye madini ya potasiamu na magnesiamu pamoja na vitamini B. Jifunze zaidi ili kujua namna ya kuandaa vya vyakula hivi na kuvitumia kwa manufaa zaidi; kwa maelezo zaidi usisite kutembelea kwenye website yetu; jifunzeafya.co.tz hapa utajifunza aina nyingi za sharubati/juisi zitakazokusaidia.
- MCHANGANYIKO WA NDIZI, EMBE, MAZIWA YA MCHELE, KIINI CHA NGANO NA MDALASINI
Kabla ya kuanza maandalizi hakikisha unanawa mikono kwa maji tiririka na sabuni
- Andaa ndizi 2 na embe 1 kwa kuvimenya
- Changanya kwenye maziwa ya mchele uliyotengeneza vikombe 2 vya mls 250 kisha weka kijiko kimoja cha ngano
- Saga mchanganyiko huo kwenye blenda mpaka viwe laini, rojorojo
- Chuja na nyunyiza nusu kijiko kidogo cha unga wa mdalasini
Mchanganyiko huu unaweza kuutumia mara 3 kwa siku ili kukusaidia kushusha shinikizo la damu na kulinda mishipa ya ateri.
Tembelea ukurasa wetu ili kujifunza Jinsi ya kutengeneza maziwa yatokanayo na nafaka;
Karibu tena kwaajili ya kujifunza aina nyingine ya sharubati kwaajili ya shinikizo la juu la damu